book

Msomee Mtoto Wako kuhusu COVID-19

cover swahili 1
cover swahili 2
read

Ninakosa kila kitu kuhusu shule, hata safari ya muda wa saa mbili kwa miguu ili kufika huko.

Mimi hutumia muda wangu kumsaidia mama huku dada zangu wakicheza. Kujipa shughuli nyingi hunisaidia kutofikiri kuhusu njaa. Mimi husikiliza masomo ya shule kwenye redio wakati baba yangu hayuko nyumbani.Leo, nilimsikia baba yangu akisema kwamba huenda asiniruhusu kurudi shuleni. Dada yangu mkubwa aliolewa akiwa na miaka kumi na mbili. Nina miaka 11 tu; Nina ndoto za kuwa mwalimu. Ninahitaji kurudi shuleni.

Nina wasiwasi kuhusu dada zangu wadogo. Nina hofu kujihusu.

read2

Mwalimu wangu, Amina, amekuja nyumbani na wanaume wawili ambao sijawahi kuwaona. Wameleta sanduku lenye chakula kwa familia yetu. Nadhani wanafanya kazi kwa mashirika ya kidunia yanayosaidia watu.

Mama yangu ananipeleka mimi na dada zangu nje kuteka maji. Anasema, "Ebu tukae hapa nje kidogo; wanahitaji kuongea na baba yako."

Watatu hao wanazungumza na baba yangu kwa muda mrefu. Nashangaa wanazungumzia nini.

read3

Baba ananiita kando na kuniambia, "Nimeamua kwamba utarudi shuleni." Anaendelea kusema, "ninaweza kukuona ukiwafundisha dada zako hisabati?"

Ninafurahi sana ninapowaeleza dada zangu kuhusu maajabu ya nambari. Hata mama na baba yangu wanaamua kushiriki. Ninaamini nitakuwa mwalimu.

Huku nikiwa na hisia za furaha na matumaini ndani ya moyo wangu, ninakula kipande changu cha chapati na kuota juu ya maisha yangu ya baadaye.

read4

------------

read5

Tuko nyumbani wakati wote. Si rahisi. Ninajaribu kuendelea na "masomo ya mbali," kama mwalimu wangu anavyoita masomo yetu kwenye kompyuta, lakini wakati mwingine nina mawazo mengi.

Nico na Felipe, ndugu zangu wadogo mapacha, hulia sana. Jambo hili linamkasirisha sana baba. Anakasirika na kumkorofisha mama. Ninachukia jambo hili linapotokea. Mama anasema kwamba baba ana wasiwasi juu ya biashara yake. Anajaribu kunifariji kwa kusema "Kila kitu kitarejea kawaida, na tutakuwa sawa mara jambo hili litakapomalizika."

Ninatumai anachosema ni sahihi. Hali katika familia yangu si kama kawaida tena.

read6

Siku inayofuata nina mawazo mengi wakati babu yangu anapopiga simu. Ninaogopa atasikia Nico na Felipe wakilia, na sauti kubwa ya Baba nyuma. Babu anauliza, "Kuna nini mbaya, Gaby?".

Siwezi kujizuia; Ninamwambia kwamba wazazi wangu wana mfadhaiko na wanapigana sana. Mapacha wanalia kila mara. Sioki tena na baba yangu. Nimekosa harufu. Ninakosa kutembea naye chini ya miti ya Jakaranda huku nikimpa hadithi zangu za shule na kula biskuti zetu tulizooka.

Babu anasema, "Gaby, nina wazo la mradi wako wa darasani. Mbona hatuandiki hadithi kuhusu jinsi siku hizi zimekuwa unaweza kuchora."

read7

"Babu yako alipiga simu," Mama anasema. Ananikumbatia na kunong'ona, "Baba yako nami tungependa kuona hadithi yako."

Ninamaliza kuwasomea, nao wanakaa kimya. Baba anamkimbilia Mama na kumwambia, "samahani" na kumkumbatia. Ananigeukia na tabasamu kubwa usoni, "Gaby, mbona tusioke biskuti?"

Ninapoimba na kuoka, hisia zangu za kawaida zinarudi. Nikiwa na hisia za furaha na matumaini, ninaamua kushiriki hadithi yangu na mwalimu wangu na wanafunzi wenzangu katika somo langu lijalo.

read8

----------------

read8

Wiki kadhaa zimepita tangu tuanze kusomea nyumbani. Mwalimu wangu alihakikisha kwamba nilipeleka vitabu na vitu vyangu nyumbani, ikiwa ni pamoja na fidla yangu, kabla ya shule kufungwa. Mambo yamekuwa magumu. Nyanya amekuwa mgonjwa sana.

Ninaweza kuona wazazi wangu wana wasiwasi. Mimi pia nina wasiwasi. Hatuwezi kuzungumza na nyanya wala kumtembelea. Ninahuzunika sana. Ninatatizika kuelezea hisia zangu na sitaki kuwasumbua wazazi wangu.

Tunaishi katika nyumba ndogo kwenye fleti, lakini bado ninahisi niko peke yangu. Sina hisia zangu za kawaida.

read9

Tunapigiwa simu kuwa Nyanya ameaga dunia. Hivyo tu. Sikupata muda wa kumuaga.

Bi Rossi, jirani yetu wa karibu, anapiga simu: "Nilisikia habari, Alessandro. Pole sana." Ninakaa kimya, sina uhakika cha kusema.

Bi Rossi anaendelea kusema, "Usisahau fidla yako, Alessandro. Katika nyakati hizi, unaweza kujieleza kupitia muziki wako." Ninasema asante kwa kupiga simu na kuikata.

Ninaangalia fidla yangu kwa muda mrefu na mwishowe ninaichukua. Ninapoicheza, ninaanza kuhisi nafuu huku machozi yakitiririka mashavuni mwangu. Wazazi wangu wananiangalia, wakitabasamu.

read10

Wazazi wangu wananiambia kuwa nyanya alipenda kusikiliza muziki wangu kila wakati na kwamba ninapaswa kwenda nje kwenye roshani yetu ili nichezee mbingu.

Ninatoka nje mapema jioni na kuanza kucheza. Ninashangaa kwani majirani wengine wanatoka nje na kucheza vyombo vyao, na watu wanaanza kuimba.

Hisia zangu za kawaida zinarudi tena. Nikiwa na hisia za furaha na matumaini, ninatumai kuwa nyanya anaweza kusikia muziki wangu.

read11
Iliyotangulia Ifuatayo