clmt

Mabadiliko ya hali ya hewa husaidia magonjwa kuenea

Magonjwa mengi yanayowaua watoto duniani (ikiwa ni pamoja na malaria, kuhara na utapiamlo) husababishwa na hali ya hewa, kama mafuriko na mabadiliko ya joto.

Kwa hakika, wadudu ambao hueneza magonjwa kama vile malaria, homa ya dengue na ugonjwa wa Lyme wanaweza kuzaana katika maeneo ambayo hawakuweza mbeleni. Madimbwi ya maji yaliyotokana na mafuriko na tufani huwa maeneo ya kuzaana kwa mbu na kupe, ambazo sasa hupatikana katika nchi nyingi za kaskazini ambazo zilikuwa na baridi sana kwa wadudu hawa kuzaana.

Aidha, mambo ambayo huleta mabadiliko ya hali ya hewa (kama vile mivuke kutoka kwa magari na viwanda) hudhuru afya ya watoto sana.

Kwa mfano, vifo vinayotokana na pumu, ambao ndio ugonjwa wa kawaida sugu kati ya watoto, vinatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa hatua ya haraka isipochukuliwa.

Iliyotangulia Ifuatayo