Rain

Matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa ni yepi?

Ingawa nchi zenye utajiri na zinazokua kwa kasi ndizo zinazotumia mafuta ghafi na rasilimali nyingine kwa njia kubwa, matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa mara nyingi huleta madhara zaidi katika nchi masikini, ambako watu wengi tayari wanakabiliana na ukosefu wa chakula na maji na magonjwa kama kipindupindu, ambayo huenea kwa urahisi zaidi wakati majanga ya asili kama mafuriko au dhoruba yanahatarisha miundo msingi ya maji na usafi wa mazingira.

Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri mambo mengi ya maisha yetu hivi kuwa yamebadilika kutoka suala la 'mazingira' na kuwa suala linalohitaji ujuzi wa pamoja katika maendeleo endelevu, uhifadhi wa nishati, na afya na ustawi wa watoto.

Hii ni baadhi ya mifano:

- Kupata maji safi ni muhimu katika maisha, afya na upataji riziki. Mabadiliko ya hali ya hewa yanatarajiwa kuleta ukame zaidi, mafuriko na kufurika kwa bahari, ambako kutafanya kupata maji safi kuwa vigumu zaidi.

- Usalama wa chakula unaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Ukame, mabadiliko ya joto, mioto ya misitu, matukio mabaya ya hali ya hewa, wadudu, magonjwa na mafuriko yanaweza kuharibu mazao ya chakula. Kuongezeka kwa utapiamlo huhatarisha afya na maisha ya wanawake na watoto na huongeza matatizo ya watu walio na VVU wanaotumia dawa za kupambana na virusi vya ukimwi, kwani lishe bora ni muhimu kwa ufanisi wa tiba hii.

  • Matokeo wazi ya mabadiliko ya hali ya hewa ni familia zilizoondolewa sehemu zao na kuhamia maeneo mengine, ambayo mara nyingi huwa na athiri mbaya kwa watoto. Katika hali hizi, watoto wanakabiliwa na hatari kubwa ya unyanyasaji na kuuzwa kwa njia haramu. Baada ya majanga, watoto wanaweza kutolewa shuleni na kufanyishwa kazi ili kusaidia familia zao kunawiri tena.

- Magonjwa kama vile malaria, homa ya dengue na ugonjwa wa Lyme yanayoenezwa na wadudu, pia yanaathiriwa na mabadiiliko ya joto kwa sababu wadudu wanaweza kuzaana katika maeneo ambayo hawakuweza mbeleni. Madimbwi ya maji yaliyotokana na mafuriko na tufani huwa maeneo ya kuzaana kwa mbu na tiba, ambazo sasa hupatikana katika nchi nyingi za kaskazini ambazo zilikuwa na baridi sana kwa wadudu hawa kuzaana.

- Huongeza athari za matukio ya hali ya hewa inayohusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambazo pia huwatia watu katika hatari, mara nyingi huharibu maeneo wanayoishi na kufanya kazi na kisha husababisha uharibifu wa mazao, kuchafuka kwa chanzo cha maji na familia zilizotengana.

- Moshi na mivuke kutokana na utumiaji wa mafuta ghafi katika nyumba, mabasi, magari na viwanda huongeza uzalishaji wa gesi chafu, na husababisha mabadiliko ya hali ya hewa kuwa mbaya zaidi, huku pia ikichafua hewa tunayopumua na kusababisha matatizo ya afya.

Iliyotangulia Ifuatayo