c2ed102b730945c6a1e3149da6c66558

Kazi ninayoitiwa ipo kweli?

Mtu fulani amenitumia ujumbe wa kuniitia kazi. Wamenitaka nikutane nao ana kwa ana. Nifanye nini?

  • Uliwahi kuomba kazi au kuzungumza na mtu yeyote kuhusu kazi? Kama hukuwahi kufanya hivyo, huo unaweza kuwa ni ujumbe wa kitapeli – kuwa mwangalifu.
  • Chunguza kidogo kuhusu kampuni au shughuli unayoitiwa – tafuta taarifa hizo kwenye intaneti au muulize rafiki yako.
  • Unapaswa kuwa mwangalifu pale unapokwenda kukutana kwa mara ya kwanza na mtu usiyemjua na ambaye umemfahamu kupitia Intaneti.
  • Siku zote panga mkutane sehemu yenye makutano ya watu (kama kwenye maduka makubwa).
  • Siku zote mfahamishe rafiki yako au mwanafamilia kuhusu mahali unakokwenda na mtu unayekwenda kukutana naye.
  • Ni vyema zaidi kama utamwomba rafiki yako au mwanafamilia akusindikize.

Kidokezo kinachofuata kuhusu Intaneti:

Iliyotangulia Ifuatayo

Maoni 0