33efd68aa8794afcba2bb0448cf54d30

Ni siri yako

Ni kwanini niwe na nywila kwa ajili ya baadhi ya tovuti ninazotaka kutumia?

  • Nywila husaidia kulinda taarifa zako binafsi pamoja na akaunti zako za barua pepe au za mitandao ya kijamii.
  • Kamwe usichangie nywila yako na mtu mwingine.
  • Nywila imara na salama haina budi kuwa na herufi, namba na alama.
  • Nywila isiyofaa ni kama vile jina lako, tarehe yako ya kuzaliwa , au “12345”. Ubaya wake unatokana na ukweli kwamba ni rahisi kwa mtu kubahatisha nywila yako na kufanikiwa kuingia kwenye akaunti yako.
  • Usitumie nywila ya aina moja kwa akaunti zako zote.
  • Badili nywila yako kila baada ya miezi michache.

Kidokezo cha Intaneti kinachofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo

Maoni 0