0e4c9a8273174ebb944a2cb77ea8723b

Unamfahamu mtu anayekuingiza?

Mtu fulani alinitumia ombi la urafiki – lakini simfahamu mtu huyo, napaswa nifanye nini?

  • Wakati mwingine watu hupenda kuwa na mawasiliano ya kimtandoa na marafiki wengi katika mitandao ya kijamii hivyo watu hao hutuma maombi mengi ya urafiki kwa watu wasiowafahamu.
  • Kabla hujakubali ombi la mtu unapaswa kwanza kupitia profaili (sifa) zao – jaribu kubaini watu hao ni akina nani. Kuna marafiki zako wanaowafahamu? Mnatoka katika mji mmoja?
  • Usiwakubalie maombi yao kama hupo tayari kushirikiana nao taarifa zako binafsi.Usijione kama unalazimishwa kufanya hivyo.
  • Hakikisha unakoweka taarifa zako binafsi ni salama ili mtu wa aina hiyo asiweze kuzipata endapo hupendi azipate.
  • Zingatia pia kuwa wakati mwingine katika intaneti watu hudanganya ili waonekane tofauti na walivyo.

Kidokezo cha Intaneti kinachofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo

Maoni 0