251e1edb43244ab7a73996c32a90f6e7

Kupokea ujumbe wa kujishindia fedha?

Nimepokea ujumbe kutoka kwa mtu fulani kuwa nimejishindia fedha au tuzo – napaswa nifanye nini?

● Kama unatumia intaneti upo uwezekano mkubwa kupata barua pepe au ujumbe wa maandishi ukikuambia kuwa umejishindia fedha au tuzo kama vile simu ya kiganjani au safari ya kwenda mapumzikoni.

● Au, wakati mwingine ujumbe wa aina hiyo unaweza ukawa ni wa kukuomba umsaidie mtu fulani kutunza fedha zake.

● Kwa kawaida wanaotuma ujumbe wa aina hiyo watakuomba uwapatie taarifa zako mbalimbali kama vile namba yako ya akaunti ya benki au ya kitambulisho. ● Ujumbe wa aina hiyo ni utapeli.

● Haiyumkiniki kujishindia kitu fulani bila kushiriki shindano lolote.

● Usibofye katika maungio ndani ya barua pepe za watu usiowajua.

● Usidhubutu kutoa nywila yako au taarifa zako nyingine binafsi (kama namba ya kitambulisho, anuani au taarifa za kibenki ) kwa watu usiowafahamu.

Mada inayofuata

Iliyotangulia

Maoni 0