Kuhusu Intaneti ya Mambo Mazuri

Intaneti ya Mambo Mazuri, "Internet of Good Things (IoGT)" ni seti ya vyanzo vya kimtandao vya taarifa na programu zinazotolewa bure kwa matumizi ya simu za kiganjani ili kukupatia mambo mazuri ya maisha yako kwa kukuwezesha wewe na jamii yako kupata habari za kielimu na za za masuala muhimu kwa maisha yako.

Mada na masuala ya Intaneti ya Mambo Mazuri ni pamoja na afya ya uzazi, usafi, taarifa za matukio ya dharura yanayohusu magonjwa kama vile Ebola, Polio na Kipindipindu, VVU, na ushauri wa masuala ya ngono kwa vijarunga, usalama wa intaneti, mbinu za kuwa mzazi bora, na mambo mengine mengi.

Kwa kujiunga na Intaneti kwa Mambo Mazuri, vijarunga, mama , baba, na wanafamilia wengine, wakufunzi wa afya, walezi na jamii wanaweza kupata habari mahususi zilizoandaliwa kwa ajili yao, za kisasa, na za ubora unaoendana na mazingira yao ya malezi, habari zitakazowafikia moja kwa moja katika simu zao za viganjani wakati wowote bila gharama.

Mtandao wa Mambo Mazuri: Ishi Vizuri Zaidi Leo