Hadithi za Uongo
Ukweli
Virusi vya Corona vyaweza kusambazwa bila kujali hali ya hewa. Uzuizi bora ni kunawa mikono yako mara kwa mara na maji na sabuni au bidhaa za pombe.
Ukweli
Watu WASIO na dalili, ikiwemo watoto wanaweza sambaza virusi. Kwa sababau hii, ni muhimu kupunguza mawasiiliano na kunawa mikono yako mara kwa mara.
Ukweli
Mpaka leo hakujakuwa na habari wala ushahidi wa kupendekeza kwamba virusi vipya vya Corona vinaweza kusambazwa na mbu.
Ukweli
Bado hakuna chanjo inayoweza kuzuia virusi vya Corona wala dawa inayoweza kuitibu.
Ukweli
Antibiotiki haziwezi fanya kazi dhidi ya virusi ila tu bakteria. Matibabu tofauti yanatumika kumudu dalili.
Ukweli
Kila mtu anaweza kuambukizwa virusi. Wazee na watu walio na hali zilizokuwepo awali (kama vile ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo) wako hatarini zaidi.
Ukweli
Ingawa kesi za kwanza za COVID-19 zilikuwa nchini China, ugonjwa huu sio maalum kwa kundi ama eneo moja. Virusi havifuati mipaka ya kijiographia, kabila, umri, uwezo, au jinsia.
Ukweli
Kunyunyuzia pombe au klorini mwili wako wote haitaua virusi ambavyo tayari vimeingia mwilini mwako. Kunyunyuzia vitu hivi kunaweza kuwa na madhara. Tumia hivi viua viini kusafisha sehemu kama ilivyoshauriwa.
Ukweli
Kila mtu anaeza saidia kulinda familia na marafiki kutokana na kuugua.
UNAEZA saidia kuachisha kuenea kwa ugonjwa kwa kufanya mazoezi ya umbali na watu, kuosha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji. kutoguza uso wako, kupiga chafya na/au kukohoa kwa kiwiko kilicho kunjwa, na kukaa nyumbani kadri iwezekanavyo.