Jinsi ya kutekeleza malezi katika nyumba na jamii zenye idadi kubwa ya watu
Inaweza kuwa vigumu zaidi kudumisha usalama wa familia yako ikiwa unaishi katika sehemu yenye watu wengi. Unaweza kuchukua hatua hizi.
1. Salia mahali ulipo.
- Punguza kuondoka na kuingia nyumbani Ondoka tu nyumbani kutekeleza shughuli muhimu kama vile kutafuta chakula na huduma za matibabu
2. Fanya mazoezi kila siku.
- Wahimize watoto kuwazia mazoezi ya mwili yanayowazuia kutangamana na watu wengine nje
- Kuruka, kucheza dansi, kukimbia katika miviringo kunaweza kufurahisha!
3. Shiriki majukumu.
- Jaribu kushiriki majukumu ya nyumbani, malezi ya mtoto, na majukumu mengine miongoni mwa wanafamilia
- Unda ratiba ya “wakati wa kazi” na “wakati wa kupumzika”pamoja na watu wengine wazima nyumbani mwako.
- Unaweza kuomba usaidizi ikiwa una mfadhaiko na unahitaji kupumzika!
4. Furahia kunawa mikono na kudumisha usafi!
- Huenda ni vigumu kupata sabuni na maji, lakini ni muhimu sana kudumisha usafi, haswa nyumbani palipo na watu wengi ambapo viiini vinaweza kuenea kwa urahisi!
- Jaribu kuhakikisha kuwa kila mwanafamilia ananawa mikono kila inapowezekana
- Waruhusu watoto kufunzana jinsi ya kunawa mikono
- Wahimize watoto kutogusa nyuso zao
5. Wasaidie watoto wako kukaa mbali na watu wengine
- Waelezee watoto wako kuwa wana jukumu muhimu la kuidumisha afya yao na ya jamii kwa kukaa mbali na watu wengine kwa muda
- Wapongeze watoto wako wanapojitahidi kukaa mbali na watu wengine
6. Pumzika.
- Unapohisi mfadhaiko au hasira, pumzika! Kupumua kwa undani mara tatu kunafaa zaidi.
- Asante kwa kusoma! Bonyeza kiungo kilicho chini ili ushiriki maoni yako kuhusu vidokezi hivi vya ulezi.