Why is it important to play and interact with my baby.jpg

Kwa nini ni muhimu kucheza na kushirikiana na mtoto wangu?

Watoto huwa wadadisi tangu wanapozaliwa. Wanataka kujifunza na kuelewa dunia yao. Akili za watoto hukua haraka zaidi katika miaka tano ya kwanza maishani mwao. Mahusiano katika miaka hizi huathiri jinsi akili ya mtoto utakavyokua, na mafunzo ya mapema huandaa mtoto kufanikiwa shuleni. Kwa hivyo, mahusiano mazuri katika miaka hizi za mapema husaidia akili ya mtoto kukua vizuri. Ubongo unapofanya kazi ndivyo uwezo wake unaimarika. Watoto wanapocheza, ubongo wao hufanya kazi sana.

Watoto hupenda kucheza na hivi ndivyo wanajifunza. Kwa mfano, mtoto akicheza mchezo wa kuficha uso wake (peekaboo) kwa kujifunika na shati au leso yako. Au mtoto wa miaka mbili anayeiga unvyosema au kutenda. Michezo hizi hupea nafasi nyingi kwa watoto kujifunza na kukuza ujuzi upya. Wakati watoto wanacheza, wao hutumia hisia zao zote (kusikia, kuona, kuonja, kugusa, kunusa na kusonga) kukusanya taarifa kuhusu dunia yao. Wanapanga taarifa hii kuelewa maisha yao, ya wengine, na dunia yao.

Kupitia mahusiano mazuri na huduma bora, furaha na michezo, watoto wataweza kukuza ujuzi upya wa kuongea na kufikiria, kusonga na kufanya, kuhisi na kujifunza kuhusu wao wenyewe na jinsi ya kuishi vyema na wengine.

Ifuatayo