Kuhusu Chanjo
Chanjo huokoa maisha ya watu milioni 2-3 kila mwaka. Popote watoto hawajachanjwa, maisha yao na jamii zao ziko hatarini.
Chanjo ni nini?
- Chanjo ni sindano na matone ambayo hulinda dhidi ya magonjwa makubwa.
- Dawa husaidia watu kupata nafuu wanapougua. Chanjo huzuia watu kutougua kimsingi.
- Chanjo nyingi hupewa watoto kwa sababu ni rahisi kwa watoto kuugua, lakini chanjo nyingi hulinda kwa maisha yote.
- Kila chanjo inalinda dhidi ya ugonjwa fulani kwa hivyo ni muhimu kupata chanjo zote.
Chanjo hufanyaje kazi?
- Chanjo zinampa mtoto wako nguvu zaidi dhidi ya magonjwa hatari.
- Chanjo hufundisha mwili wa mtoto wako kutambua na kukumbuka vijidudu vinavyowafanya waugue. Wakati mtoto aliyepewa chanjo anapokutana na kijidudu hatari, mara moja inagundua tishio na kupambana nalo.
- Chanjo hufunza mfumo wa kinga kupambana na magonjwa."
Mambo 5 Ya Uhakika Kuhusu Chanjo
Chanjo huwa salama na yenye ufanisi.
Chanjo huzuia magonjwa hatari.
Chanjo hutoa kinga bora kuliko maambukizo ya asili.
Chanjo zilizochanganywa ni salama na zina faida.
Tukiwacha chanjo, magonjwa yatarudi.