Mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia usalama wa chakula
Usalama wa chakula unaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kama ukame, mabadiliko ya joto, mioto ya misitu, matukio mabaya ya hali ya hewa, wadudu waharibifu, magonjwa na mafuriko yanaweza kuharibu mimea ya chakula. Hili linazidisha hali ya ukosefu wa chakula duniani uliyopo tayari, kwani mazao ya kawaida ya chakula kama vile mchele, ngano na mahindi huathirika.
Kuongezeka kwa utapiamlo huhatarisha afya na maisha ya wanawake na watoto na huongeza mashaka zaidi kwa watu wenye VVU, ambao wanatumia dawa za kupambana na virusi vya ukimwi, kwani lishe bora ni muhimu kwa matibabu haya kufanikiwa.
Wanasayansi wanakadiria kuwa ongezeko la joto na mvua usiyofuata mkondo wa kawaida huenda kukapunguza uzalishaji wa mazao katika maeneo mengi yenye hali mbaya ya hewa. Katika nchi zinazoendelea, hili litaacha mamia ya mamilioni ya watu bila uwezo wa kuzalisha au kununua chakula cha kutosha.
Aidha, mabadiliko ya hali ya hewa ya mazingira yanafanya iwe vigumu kupata vyanzo vya mwitu vya chakula, kwa vile ujuzi wa watu wa kujua wakati na mahali pa kuwinda, kuvua samaki na kupata chakula na mimea unaendelea kokosa kuwa wa kutegemewa.
Lakini mipango rahisi inaweza kuwa ya manufaa zaidi. Katika kijiji cha Alikinkin, Niger, bustani za jamii ni chemchemi za kuvutia na chanzo cha chakula, na husaidia watoto kuepuka athari mbaya zaidi za ukosaji wa lishe bora.