Hatujachelewa!
Mabadiliko ya hali ya hewa ni suala la kimataifa ambalo litaathiri maisha ya kila mtu.
Hatuwezi kukomesha kabisa mabadiliko ya hali ya hewa ambayo tayari yanatokea, lakini tunaweza kuchukua hatua ili kupunguza kiwango cha sasa na cha baadaye cha mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuandaa jamii zetu kukabiliana na matokeo ya mabadiliko haya.
Tunaweza kuchukua hatua ya kibinafsi na ya pamoja ili kupunguza kiasi cha nishati tunachotumia na kiwango cha dioksidi ya kaboni ambayo tunatoa.
Tunaweza kuchukua hatua ili kupunguza uwezekano wa jamii zetu kuathirika na upungufu wa chakula na maji, na kuenea kwa magonjwa.
Vitendo vingine vina manufaa kadhaa: kwa mfano, kujenga bustani shuleni kunaweza kusaidia kukabiliana na kiwango cha gesi chafu, kwa kuwa mboga zilizopandwa huko zinaweza kutumika badala ya mazao yanayoletwa kutoka mbali kwa kutumia magari au ndege. Kunaweza pia kuongeza usalama wa chakula kwa jamii..