Ongeza ufahamu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa!
Unajua umuhimu wa kulinda mazingira!
Hapa kuna njia unazoweza kutumia kueneza habari:
-
Andika makala kwa gazeti la shule au eneo lako.
-
Ifunze familia yako, marafiki na jamii kuhusu madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na jinsi vikundi tofauti (wanawake na wanaume, matajiri na maskini, vijana na wazee) vinaathirika kwa njia tofauti.
-
Fikiria kuhusu kuandaa warsha au kujitolea kutoa mafunzo katika mikutano na sherehe zinazofanyika.
-
Tengeneza bango, karatasi la matangazo au video inayoonyesha tatizo maalum la mazingira ulilolitambua katika jamii yako.
-
Panga mchezo wa kuigiza kwa jamii ya eneo lako, mkiigiza kuhusu madhara makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na vitendo ambavyo watu wanaweza kuchukua ili kupunguza madhara kwa mazingira.
-
Panga tukio la umma ambalo linavutia watu kwa vitendo vyako ulivyochukua ili kupunguza utoaji wa vichafuzi: Waalike viongozi wa mitaa kwa sherehe ya kupanda miti; unda jiko jua katika mahali pa umma na upike chakula maalum cha mtaa wako.
-
Shuleni, uungana na wanafunzi wengine na viongozi wa shule kuendeleza na kutekeleza mpango wa kuhifadhi nishati.
-
Hutubia mkutano kwa darasa lako au shule.
-
Panga tukio maalum, mkutano, tamasha au tukio la michezo. Hili linaweza kufanyika siku moja na matukio duniani kote kama vile Siku ya Mazingira ya Dunia (Juni 5), Siku ya Dunia (Aprili 22), Siku ya Kupunguza Majanga (Jumatano ya pili ya Oktoba), Siku ya Maji Duniani (Machi 22) au Siku ya Kimataifa ya Vijana (Agosti 12).
-
Andika barua kwa wizara za mazingira za eneo lako na za kitaifa. Tumia sauti yako na ujuzi kuzishawishi.