Punguza utoaji wako wa vichafuzi!
Kupunguza utoaji wa dioksidi ya kaboni katika maisha yako ya kila siku ni rahisi sana!
Hii ni mifano ya kile unachoweza kufanya:
-
Tumia usafiri wa umma, endesha baiskeli au tembea mara nyingi zaidi, na wahimize wengine kufanya hivyo, pia.
-
Zima taa na vifaa vya umeme wakati huzitumii.
-
Ziba uvujaji wa hewa kwenye madirisha na milango, na uweke mikeka kwenye sakafu yako ili uweze kuweka nyumba yako ikiwa na joto, huku ukipunguza kidhibiti joto chako ili kuokoa nishati.
-
Nunua nguo zilizotumiwa na vitu vingine, na utoe kama msaada vitu ambavyo huvitumii tena.
-
Nunua bidhaa ambazo zimeundiwa au kukuzwa nchini badala ya kusafirishwa au kuletwa na ndege kutoka mbali.
-
Jifunze jinsi ya kukuza chakula chako mwenyewe, na usaidie wengine kujifunza.
-
Kula nyama kidogo, kuku na samaki, ambazo hutumia nishati zaidi kukuza kuliko vyakula vya mimea.
-
Unda jiko jua (angalia makala maalamu: Unda jiko jua!
-
Panda miti au uandae sherehe ya kupanda miti.
-
Hamasisha familia na wanajamii kutenda mambo haya, pia.