Wewe ndiwe suluhu!
Huku mazingira ya kimataifa yakiendelea kuharibika kwa kasi zaidi, hili linaathiri watoto na vijana zaidi! Watoto na vijana wenye umri mdogo wenye ufahamu wa mazingira ndio mawakala wakubwa wa mabadiliko na ulinzi wa muda mrefu wa mazingira na uongozi wa dunia.
Zaidi ya asilimia 46% ya wakazi wa dunia wana umri wa chini ya miaka 25!
Maamuzi unayofanya yanaweza na yatabadili mustakabali wa dunia yetu.
Hivyo jihusishe katika ulinzi wa mazingira yako, anza kujifunza na uzungumzie jambo hili zaidi. Tayari unaleta mabadiliko! Watoto wanaweza kubadili ulimwengu wao wenyewe! Watu wakubwa wanapaswa kukuza ushiriki wa watoto katika mipango ya mazingira, kuimarisha vilabu na mitandao ya watoto, na kuyazingatia maoni ya watoto katika mchakato wa maendeleo, wa eneo lao, wa kitaifa na wa kimataifa.
Katika Afrika, ambako idadi wa watoto inatarajiwa kukua kuliko mbeleni, watu wanoatunga sera wana fursa ya nadra sana ya kuwekeza katika watoto ili bara, na ulimwengu, uweze kunufaika na mabadiliko ya idadi ya watu katika Afrika . Pata zaidi kwa kusoma taarifa ya UNICEFGeneration 2030 | Africa (external link data charges may apply)Generation 2030 | Africa