Phys Health 1.png

Kuishi vizuri na Virusi Vya Ukimwi

Ikiwa unaishi na Virusi Vya Ukimwi, unaweza kuishi maisha ya furaha, marefu na yenye mafanikio kama marafiki zako ambao hawana VVU. Lakini kujifunza jinsi ya kuishi vizuri na VVU kunaweza kumaanisha kuwa unakabiliana na changamoto nyingi zaidi kuliko marafiki zako na kunamaanisha utunze afya yako ya kimwili na kiakili. Kunamaanisha kufikiri juu ya:

Matibabu ya Virusi Vya Ukimwi

Kuanza tiba dhidi ya VVU (ART) mapema iwezekanavyo husaidia kudhibiti virusi na kuzuia kueneza maambukizi kwa wengine.

  • Pata matibabu yako ya VVU kila siku.
  • Ikiwa una wasiwasi kuhusu athari ya matibabu au una maswali yoyote kuhusu matibabu yako, zungumza na daktari wako.
  • Ni haki yako kuamua kama utapata matibabu ya VVU, lakini kamwe hupaswi kuacha kutumia matibabu yako bila kwanza kujadiliana na daktari wako. Inaweza kuwa hatari sana kwa afya yako.

U=U

ART inapofanya kazi vizuri, inaweza kupunguza kiwango cha virusi hadi kiasi ambacho vipimo haviwezi kupima - hii inaitwa 'kutoonekana'. Ikiwa 'huonekani', 'huwezi kuenezwa'. Hii ina maana kwamba ingawa una VVU, inadhibitiwa na matibabu na huwezi tena kuisambaza. Ili kujua jinsi ART yako inavyofanya kazi unahitaji kupimwa damu mara kwa mara ili kubaini kiwango cha virusi vyako.

Kula vizuri na kufanya mazoezi

Ni muhimu kula vizuri ili kuhakikisha kuwa ART yako inaweza kufanya kazi vizuri. Chakula kinachofaa kinaweza kukusaidia kudumisha uzito wenye afya na kuupa mwili wako vitu vyote unavyohitaji. Mazoezi yanaweza pia kusaidia kukupa siha na afya nzuri na ni muhimu kwa afya ya akili pia. Pata maelezo zaidi kuhusu lishe na mazoezi.

Afya ya akili

Kuishi na VVU kunaweza kuathiri afya yako ya akili. Kuelewa uaguzi uliofanyiwa, kuamua ni nani utakayeeleza na kukabiliana na unyanyapaa vinaweza kuleta mahangaiko na wasiwasi mwingi. Hali hii inaweza mfadhaiko na wasiwasi na katika hali zingine msongo wa mawazo. Ni muhimu kuwa na watu wa kuzungumza nao ambao wanaweza kukusaidia kudhibiti hisia na matatizo mbalimbali ambayo huenda ukakumbana nayo. Pata maelezo zaidi kuhusu Kuishi na VVU na afya yako ya akili.

Virus Vya Ukimwi na UVIKO-19

Ni muhimu kwamba kila mtu afuate ushauri wa kujikinga dhidi ya UVIKO-19 na ikiwa utaonyesha dalili za maambukizi ya UVIKO-19 lazima upate usaidizi. Bado hatujui ikiwa watu wanaoishi na VVU wanaopata UVIKO-19 wanakuwa wagonjwa zaidi kuliko wale ambao hawana VVU. Lakini tunajua kuwa watu walio na mfumo dhaifu wa kinga wana uwezo mdogo wa kukabiliana na maambukizi - ikiwa ni pamoja na UVIKO-19. Hii ndiyo sababu ni muhimu sana kuendelea kutumia ART zako ili kuhakikisha kuwa mfumo wako wa kinga uko imara kadri iwezekanavyo. Bado lazima uende kwa miadi ya matibabu. Hakikisha kuwa unafuata ushauri wa kujikinga na UVIKO-19 ikiwa unasafiri kwa uchukuzi wa umma na ukienda kliniki.

Katika nchi nyingi watu wanaoishi na VVU wanapendekezewa kupata chanjo ya UVIKO-19 mara tu inapopatikana.

Iliyotangulia