Kuhusu Virusi Vya Ukwimi
VVU ni nini?
VVU inawakilisha Virusi vya Ukimwi. Ni virusi vinavyoshambulia mfumo wa kinga ya mwili, na kuifanya kuwa vigumu zaidi kupambana na maambukizi.
UKIMWI ni nini?
VVU na UKIMWI ni tofauti. Bila matibabu, VVU inaweza kuharibu sana mfumo wa kinga ya mwili na kuufanya kuwa dhaifu sana kuweza kupigana na maambukizi. Hii inaitwa UKIMWI, ambayo inasimamia Upungufu wa Kinga Mwilini. UKIMWI ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na VVU. Kwa kuwa sasa watu wengi wanapokea matibabu ya VVU, ni watu wachache wanaokufa kutokana na UKIMWI
Mtu hupataje VVU?
Huwezi ‘kupata’ VVU, kama vile unavyoweza kupata homa. VVU hupitishwa kupitia viowevu 4 tu vya mwili:
- Damu
- Shahawa
- Maji ya uke
- Maziwa ya mama
Watu wengi hupata VVU kwa kufanya mapenzi bila kinga (ngono bila kondomu).
Njia pekee ya kujua kama una VVU ni kwa kupimwa. Huwezi kujua kwa kumtazama tu mtu kama ana VVU. Watu wengi walio na VVU hawana dalili zozote, hasa ikiwa wanapata matibabu.
Unawezaje kuzuia VVU?
Kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kuzuia VVU:
- Tumia kondomu kila wakati unaposhiriki ngono.
- Msitumie kwa pamoja sindano, sirinji na vifaa vingine vya kudungia.
- Ikiwa una VVU, kupata matibabu ya VVU kunaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya VVU kwa watu wengine, ikiwa ni pamoja na mtoto ambaye hajazaliwa kama una mimba.
- Katika baadhi ya maeneo, kuna dawa za VVU ambazo zinaweza kutumiwa kabla na baada ya kujamiiana ili kuzuia maambukizi ya VVU. Hizi huitwa PrEP (kifupi cha kinga kabla ya kupitia hali ya kuweza kuambukizwa) na PEP (kinga baada ya kupitia hali ya kuweza kuambukizwa).
Ili kupata maelezo zaidi, angalia marejeleo haya: