Phys Health 3.png

Uzuiaji Mimba na Kondomu

Kuzuia mimba zisizohitajika na magonjwa ya zinaa (STIs), pamoja na VVU, kunamaanisha kwamba unaweza kuwa huru na kufurahia ngono bila wasiwasi! Kuna visa vingi visivyo kweli kuhusu uzuiaji mimba na ujauzito - kufanya ngono ukiwa umesimama au kuosha sehemu zako za siri kwa maji ya limau ni mambo ambayo hayatakuzuia kupata mimba au kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono. Hakikisha una kizuia mimba kabla ya kushiriki ngono.

Uzuiaji Mimba na Kondomu

Chagua mbinu sahihi ya uzuiaji mimba kwako na kwa mpenzi wako - kila moja ina faida na changamoto.

  • Kondomu hutoa ‘ulinzi maradufu,’ huzuia mimba na magonjwa ya zinaa, kama vile VVU. Kuna aina mbili za kondomu: zile zinazovaliwa na wanaume na zingine zinazovaliwa na wanawake. Kondomu za kike huitwa femidoms.
  • Kondomu za kiume hupatikana kwa urahisi - unaweza kuzinunua kwa bei nafuu kutoka kwa vioski na maduka ya dawa na uzipate bila malipo kwenye kliniki za afya.
  • Njia zingine za udhibiti wa uzazi huzuia tu mimba; hizi wakati mwingine huitwa uzazi wa majira. Uzazi wa majira ni wa wanawake pekee. Baadhi ya mbinu hudumu miezi kadhaa (k.m. vipandikizi vya homoni, sindano za kuzuia mimba, vifaa vya ndani ya uterasi au IUD), huku zingine zikitumiwa kila siku (k.m. tembe za kuzuia mimba).
  • Ikiwa umefanya tendo la ndoa na hukutumia mbinu za kuzuia mimba, mbinu za dharura za kuzuia mimba (mara nyingi huitwa ‘tembe za asubuhi baada ya tendo’) zinaweza kuchukuliwa baada ya kufanya mapenzi bila kinga ili kuzuia mimba. Zinapaswa kumezwa haraka iwezekanavyo na ndani ya saa 72 au 120 kulingana na chapa.
  • Nenda kwenye kituo chako cha afya ili upate ushauri na mbinu za uzuiaji mimba. Usitegemee tiba za nyumbani, hazifanyi kazi!

Ngono Salama

Wakati mwingine utakapofanya ngono, unapanga kutumia kondomu?

Hiari
Chagua moja

Umri wa ridhaa

Ikiwa hujatimiza umri wa kutoa ridhaa (umri unaoruhusiwa kisheria kushiriki ngono), huenda ukahitaji ruhusa ya mzazi/mlezi wako ili kupata vizuia mimba. Ikiwa unashiriki ngono kabla ya umri wa ridhaa, huenda kuna sheria zinazomaanisha kuwa mmoja wenu au nyote wawili mnaweza kuwa mnatenda kosa la jinai kwa kushiriki ngono; hakikisha umefikiria juu ya kile kinachoweza kutokea. Unafikiri uko tayari kushiriki ngono? Pata maelezo zaidi kuhusu kufurahia ngono yenye afya na iliyo salama

Magonjwa ya Zinaa (STIs)

Kutumia kondomu huzuia magonjwa ya zinaa pamoja na VVU. Magonjwa mengi ya zinaa hayana dalili zozote, kwa hiyo ikiwa unashiriki ngono, ni vyema kutumia kondomu na kwenda kupimwa mara kwa mara. Ikiwa una dalili, zinaweza kuwa na uchungu na hazitaisha zenyewe. Ikiwa huhisi vizuri au mambo hayaonekani kuwa sawa, ni muhimu kuchunguzwa. Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kutibiwa iwapo utapata ushauri mapema, na huduma hizo ni za siri. Ikiwa una wasiwasi kwamba huenda wewe ni mjamzito au una ugonjwa wa zinaa ni muhimu kwenda kliniki haraka iwezekanavyo. Huduma hizi zipo kwa kila mtu na ukipimwa mapema, ndipo unaweza kupata matibabu kwa haraka na kufikiria juu ya uamuzi utakaofanya ikiwa una ujauzito.

Usiaibike - kumbuka wataalamu wa afya huona mambo kama haya kila wakati. Ni kazi yao kukutibu bila kukuhukumu na kukusaidia kuzuia na kutibu magonjwa ya zinaa.

Kwa habari zaidi kuhusu ujauzito tembelea ukurasa wetu wa ujauzito.

Iliyotangulia Ifuatayo