Sexual Health 2. png.png

Ngono na Usalama Mtandaoni

Katika ulimwengu wa kidijiti, sasa tunaweza kuwa na mahusiano mtandaoni na kufikia nyenzo kuhusu ngono na mahusiano. Hili linaweza kufurahisha, wakati ni salama na umejifikiria na kuwafikiria wengine mnapowasiliana mtandaoni na kupitia programu za kutuma ujumbe.

Utumaji wa Ujumbe na Picha za Mapenzi na Selfii

Kutuma ujumbe au picha ‘zinazohusu mapenzi’ (‘sexting’) kwa mpenzi wako kunaweza kusisimua na kufurahisha lakini kumbuka kuna sheria zinazolinda usalama wako.

  • Kutuma ujumbe kati ya vijana wasiotimiza umri wa miaka 18 mara nyingi ni kinyume cha sheria. Baadhi ya programu za simu pia zina sheria kuhusu lugha na maudhui unayoshiriki (kumbuka kampuni zinaweza kuangalia ujumbe wako, hakuna kitu ambacho ni cha faragha 100%).
  • Huenda baadhi ya watu wakapenda kujaribu ‘kutuma ujumbe na picha za mapenzi’ lakini huenda wasihisi vizuri kulitenda hilo na kamwe hawapaswi kulazimishwa kulifanya.
  • Hujui kitakachotokea kwa ujumbe au picha utakayotuma. Zinaweza kutumwa kwingine bila idhini yako. Hili hutokea sana wakati uhusiano unapofikia kikomo na watu wanataka kukufadhaisha. Fikiria jinsi ungehisi ikiwa uaminifu huu ungevunjwa.
  • Ikiwa umeahidi kuweka mambo faraghani na kufuta ujumbe lazima utimize ahadi yako pia.

Ikiwa mtu atausaliti uaminifu wako, inaweza kuwa vigumu kushughulikia hilo. Unaweza kuaibika kwamba watu wengine wanaziona picha hizo. Kumbuka haya yote si makosa yako, hakuna mtu anayepaswa kutuma kwingine vitu bila ruhusa yako. Unaweza kuripoti hili kwa tovuti za mitandao ya kijamii na kuomba ziondolewe. Itafaa ikiwa unaweza kutoa ushahidi kwa kupiga picha za skrini za tovuti ambapo zimetumwa. Unaweza kumwomba rafiki yako afanye hivi ikiwa unaona ni vigumu sana.

Hakikisha kuwa unapata usaidizi wa aina fulani ili kukabiliana na hisia ambazo huenda unazo. Kumbuka, hupaswi kamwe kuhisi kuwa unashinikizwa kutumia wengine vitu usivyotaka kutuma, hata kama mtu yeyote anajaribu kukushawishi sana kufanya hivyo.

Ponografia

Ponografia ni maudhui 'dhahiri ya ngono' ambapo watu wanaigiza ngono au vitendo vya ngono. Imekuwepo kwa namna tofauti kwa mamia ya miaka ili kutia ashiki, kuchochea na kufurahisha watu.

Baadhi ya ukweli kuihusu:

  • Ponografia huigizwa - ni mara chache sana inapoonyesha watu, uhusiano au shughuli za ngono za kweli - ni ngono ya mawazoni.
  • Kwa kawaida ponografia haionyeshi kuwa ngono inapaswa kuwa ya maelewano na salama, au kondomu hutumika.
  • Ponografia inaweza kutupa mawazo na matarajio yasiyo ya kweli, na hata yasiyoyofaa, kuhusu ngono, miili yetu na mahusiano.
  • Kwa baadhi ya vijana, taarifa pekee walizo nazo kuhusu ngono ni kupitia ponografia, na hizi zinaweza kuwapa mawazo ya kutatanisha na yasiyofaa kuhusu kile wanachotarajia na zikaathiri tabia zao.
  • Ponografia inaweza kuleta madhara ikiwa itawafanya watu wafikiri kwamba picha za watu na wanachofanya katika filamu za ngono ni jambo la kawaida.
  • Sio ponografia yote iliyo mbaya kwani kuna ponografia inayotayarishwa ambayo inaonyesha mahusiano ya aina mbalimbali. Pia kuna filamu ambapo ridhaa na matumizi ya kondomu huonyeshwa.
  • Usifikirie kuwa mwenzi wako atapenda mambo yanayofanywa katika filamu - ni muhimu kila wakati kupata ridhaa kwa shughuli ya aina yoyote ya ngono. Kumbuka haionyeshi maisha halisi!
Iliyotangulia Ifuatayo