TIps for managing period pain

Kukanusha visa kuhusu Hedhi

Hapo mbeleni hedhi ilikuwa kama fumbo. Kwa sababu hii, kulikuwa na visa vingi vilivyobuniwa kabla ya maelezo ya kibiolojia kupatikana.

Hebu tujadili baadhi ya visa hivyo:

KISA CHA 1: Wasichana ambao wako kwenye hedhi wana doa, ni wachafu au hata wamelaaniwa.

Hakuna doa au uchafu wowote kuhusu hedhi au maji ya hedhi na pia kutokwa na damu sio ishara kwamba umelaaniwa. Huu ni mchakato muhimu wa mwili na umajimaji unaotoka kwako ni mchanganyiko usio na madhara wa damu na tishu.

KISA CHA 2: Wasichana hawapaswi kuoga wakati wa hedhi.

Uongo. Kuoga, kubadilisha vifaa vyako za usafi (k.m., pedi au kisodo), na kutumia chupi safi ni sehemu muhimu za usafi mzuri wa hedhi.

KISA CHA 3: Wasichana watakuwa wagonjwa kutokana na kupoteza damu 'nyingi' wakati wa hedhi.

Hupaswi kupoteza damu nyingi hadi usababishe upungufu wa chuma. Jichunge mwenyewe na zungumza na daktari ikiwa una wasiwasi.

KISA CHA 4: Wasichana hawawezi kupata mimba wakati wa hedhi.

Si ukweli. Inawezekana kwa msichana kupata mimba ikiwa atashiriki ngono, hata wakati wa hedhi yake.

KISA CHA 5: Wasichana hawafai kwenda shuleni, kuabudu au kubarizi na wavulana wanapokuwa kwenye hedhi.

Si hivyo. Unapaswa kuendelea na maisha yako kama kawaida, mradi tu unajisikia vizuri. Beba tu sodo na uzibadilishe mara kwa mara.

KISA CHA 6: Sodo husababisha utasa.

Uongo. Sodo ni salama na mara nyingi huhitajika ili kukuweka mkavu na safi.

KISA CHA 7: Wasichana wanapopata hedhi mapema (kama umri wa miaka 10), inamaanisha wamekuwa wakishiriki ngono.

Si ukweli. Miili yote ni tofauti na kuna kipindi cha umri wa kupata hedhi yako ya kwanza. Unaweza kupata hedhi wakati wowote baada ya miaka 10 hadi mwisho wa ubalehe ukiwa na umri wa miaka 15 au zaidi.

Iliyotangulia