pollution

Uchafuzi wa hewa huzoretesha mabadiliko ya hali ya hewa zaidi

Uchafuzi wa hewa unaotoka kwa viwanda, magari na kaya, ambao ndio sababu kuu ya mabadiliko ya hali ya hewa kuliko athari zingine, unaathiri sana afya ya watoto. Uchafuzi wa hewa unaotoka kwa viwanda, magari na kaya mara nyingi huwa mbaya zaidi mijini. Kwa vile watoto wengi huishi mijini, hili linaleta tishio kubwa. Kupatwa na vichafuzi vya hewa kupitia kupumua ni jambo gumu haswa kwa watoto, kwa sababu mapafu yao ni madogo na bado yanaendelea kukua hadi wanapotimiza karibu umri wa miaka 18.

Moshi na mivuke inayotokana na utumiaji wa mafuta nyumbani, mabasi, magari na viwanda huongeza utoaji wa gesi chafu, na husababisha mabadiliko ya hali ya hewa kuwa mabaya, huku pia ikichafua hewa tunayoipumua na kusababisha matatizo ya afya. Moshi na mivuke inayotokana na matumizi ya jiko la kupikia linalotumia vitu kama kuni na makaa pia huzidisha matatizo ya kiafya ya kupumua na hutoa mivuke inayoleta madhara kwenye anga.

Ifuatayo