Miti inasaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa
Miti hutupa kivuli dhidi ya joto la mchana, huzaa matunda ambayo nichakula chetu na hufanya mazingira yawe ya kuvutia. Kukata miti kwa ajili ya kuni kunasababisha uharibifu wa misitu na huleta jangwa na kunahusishwa na utoaji wa gesi chafu na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa mtazamo wa kimazingira, miti ni muhimu: oksijeni inayotupa uhai inayotoka kwa miti huondoa uchafuzi wa hewa, hupunguza joto na huongeza unyevu kwenye hewa. Kwa kushika udongo pamoja na kuzuia kasi ya mito, miti huzuia mmomonyoko wa udongo, hudhibiti maporomoko, hupunguza ueneaji wa jangwa, hulinda maeneo ya pwani na huimarisha matuta ya mchanga. Ndege na wanyamapori wengine wanahitaji miti kwa ajili ya makao na chakula - na vilevile watoto.
Aidha, uharibifu wa miti ni suala la kijinsia na afya. Wanawake na wasichana hutumia idadi kubwa ya masaa kila siku wakitafuta kuni za kupika, na wanaathiriwa sanaa na moshi ndani ya nyumba kutoka kwa moto wa kupikia.
Uhifadhi wa mazingira kwa njia ya kupanda miti ni moja ya misingi ya maendeleo. Kwa mfano, Serikali ya Ethiopia iliweka lengo la kupanda miti milioni 20. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalifanya kazi kwa karibu na serikali kuhamasisha umma, hasa watoto na vijana, kushiriki katika changamoto hiyo.