Phys Health 2.png

Je, unafanyaje uchaguzi wa vyakula vyenye afya?

Kula vyakula vyenye virutubishi mbalimbali ni sehemu muhimu ya maisha yenye afya. Hapa kuna mwongozo:

  • Kula milo 3 kwa siku, pamoja na asusa zenye afya.
  • Ongeza faiba katika chakula na punguza matumizi ya chumvi.
  • Kunywa maji. Jaribu kuepuka vinywaji vyenye sukari nyingi. Juisi ya matunda inaweza kuwa na sukari nyingi, kwa hiyo kuchagua matunda mazima daima ni chaguo bora zaidi.
  • Kula asusa za matunda au mboga.
  • Kula kuku na samaki zaidi. Punguza ulaji wa nyama nyekundu na chagua nyama isiyokuwa na mafuta inapowezekana.

Kutana na Sahani Yangu

Phys Health My Plate.png

Aikoni ya SahaniYangu imegawanywa katika kategoria 5 za vikundi vya chakula, ikisisitiza upataji wa lishe wa vifuatavyo kwenye sahani yako:

  • Kabohaidreti - ¼ ya sahani yako.
    • Vyakula vinavyotengenezwa kwa ngano, mahindi, mchele, shayiri, au nafaka nyingine ni bidhaa za nafaka. Mifano inajumuisha ugali, ngano isiyokobolewa, mchele wa hudhurungi, na chakula kinachotoka kwa unga wa shayiri.
  • Matunda na Mboga - ½ ya sahani yako.
    • Badilisha mboga unazokula. Chagua aina mbalimbali za mboga, ikiwa ni pamoja na mboga za kijani iliyokolea, nyekundu, na machungwa, kunde (njegere na maharagwe), na mboga za wanga.
    • Tunda lolote huhesabiwa katika sehemu ya kikundi cha matunda. Matunda yanaweza kuwa mabichi, yaliyowekwa kwenye makopo, yaliyogandishwa, au kukaushwa, na yanaweza kuwa mazima, yaliyokatwakatwa au kufanywa kuwa rojo.
  • Protini - ¼ ya sahani yako.
    • Tumia protini zisizo na mafuta. Chagua nyama yenye kiasi kidogo cha mafuta au isiyo mafuta au kuku. Badilishabadilisha protini unazotumia - chagua samaki zaidi, njugu, mbegu, njegere, na maharagwe.

Kando ya sahani

  • Mafuta ya mmea yenye afya - kwa wastani. Chagua mafuta ya mboga yenye afya kama mzeituni, soya, mahindi, alizeti, karanga. Mengine, kama vile mafuta ya wanyama, huwa yameganda na yanapaswa kuepukwa.
  • Kunywa maji, kahawa au chai. Epuka vinywaji vyenye sukari, na punguza matumizi ya juisi hadi glasi ndogo kwa siku.
  • Bidhaa za maziwa na vyakula vingi vilivyotengenezwa kutoka kwa maziwa vinachukuliwa kuwa sehemu ya kundi hili la chakula. Zingatia bidhaa zisizo na mafuta au zenye kiasi kidogo cha mafuta, pamoja na zile zilizo na kalsiamu nyingi. Punguza maziwa na bidhaa za maziwa hadi mgao mmoja au miwili kwa siku.
Iliyotangulia Ifuatayo