Ngono na Mahusiano

Wakati mwingine inahisika kama kila mtu anazungumza juu ya ngono! 'Kupoteza ubikira wako' na kufanya ngono kwa mara ya kwanza kunaweza kuhisika kama jambo kubwa lakini si mashindano na ungetaka kufurahia jambo hilo. Ngono ni sehemu moja tu ya uhusiano na kushiriki ngono si thibitisho la upendo! Ujinsia unahusu mambo mengi zaidi ya ngono tu - unahusu yule tunayevutiwa naye (wavulana, wasichana, wote wawili au hakuna mtu) na shughuli zingine za kijinsia ambazo tunaweza kufurahia kwa usalama. Kila mtu ana haki ya kufurahia jinsia yake na kushiriki ngono ya kuridhiana, bila kujali mwelekeo wake wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, hali ya VVU au tofauti zingine, pamoja na watu wenye ulemavu.

Mambo ya kukumbuka kwa ngono salama na ya kufurahisha!

  • Subiri hadi ujisikie uko tayari na ufanye ngono tu ikiwa unataka - usishiriki ili uonekane "unayevutia" au kwa sababu unafikiri marafiki zako wote wanashiriki. Si mashindano! Je, unahisi kuwa tayari kimwili na kihisia? Je, unahisi umepumzika, umestarehe, na u salama? Kumbuka, unaweza kubadilisha mawazo yako wakati wowote na kusema hapana.
  • Hakikisha unaomba na kupata ridhaa ya ngono - ridhaa ni wakati mtu anasema ndiyo kwa uwazi na kwa furaha na hahisi shinikizo lolote kwa jibu lake. Pata maelezo zaidi kuhusu ridhaa hapa
  • Zungumza juu yake! Mawasiliano mazuri = ngono nzuri na salama. Ongea na mwenzi wako kuhusu jinsi unavyohisi na kile ambacho nyinyi wawili mnapenda/hampendi. Hupaswi kufanya chochote ambacho hutaki kufanya.
  • Kumbuka, unaweza kufurahia aina tofauti za ngono na njia tofauti za kuwa marafiki na wandani.
  • Hakikisha unatumia kondomu ili uweze kufurahia kufanya ngono na ili usiwe na wasiwasi kuhusu kupata mimba au magonjwa ya zinaa (STI), ikiwa ni pamoja na VVU. Unaweza kupata kondomu na mbinu za kuzuia mimba kutoka kwa kliniki ya eneo lako. Pata maelezo zaidi kuhusu uzuiaji mimba hapa
  • Kumbuka kwamba kufanya ngono kwa mara ya kwanza, kufanya mapenzi ukiwa umesimama, au ‘kutoa’ (kuchomoa uume kabla ya ‘kufikia kilele’ au kumwaga manii) hakukuzuii kupata mimba au kupata magonjwa ya zinaa.
  • Kumbuka ‘maneno haya muhimu’ – mawasiliano, ridhaa, mbinu za uzuiaji mimba na kondomu!

Consent Scenario

Tate has a friend Samuel who is always boasting about how many girls he has sex with. He tells Tate that the easiest way to get them to have sex is to pick the ones who are really drunk and give them more alcohol. Samuel proudly describes how he can do what he wants when they are sleeping or unconscious.

What should Tate do?

Chagua moja

Kukaa salama na kutahadhari

  • Kumpa mtu pesa na zawadi ili afanye mambo fulani ni aina ya hongo au udhibiti. Hali ya kukubali zawadi ili ushiriki ngono humpa mtu nguvu zaidi dhidi yako na unaweza kuhisi kutokuwa na uwezo wa kuchagua aina ya uhusiano na ngono unayoshiriki. Pata maelezo kuhusu mahusiano yenye afya.
  • Usishiriki ngono, hasa kwa mara ya kwanza, ukiwa umelewa kwa pombe au dawa za kulevya - kwa kawaida matokeo yake si mazuri na unataka kuyakumbuka! Kumbuka kwamba watu hawawezi kutoa ridhaa yao ikiwa wamelewa au wakiwa katika ushawishi wa dawa za kulevya. Pata maelezo zaidi kuhusu kujiweka salama
  • Ikiwa una wasiwasi unaweza kuwa mjamzito au una ugonjwa wa zinaa ni muhimu kwenda kliniki haraka iwezekanavyo. Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kutibiwa iwapo utapata ushauri na matibabu mapema, na huduma hizo ni za siri. Huduma hizi ni muhimu na zinapatikana kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na wakati wa UVIKO-19. Pata maelezo zaidi kuhusu ujauzito

Sex & Relationships Quiz

I am married so I don’t need to get consent for sex anymore. True or false?

Chagua moja

Iliyotangulia Ifuatayo