About Coronavirus

Kuhusu virusi vya Corona

COVID-19 ni nini?

Ugonjwa wa virusi vya Corona 2019 (COVID-19) - 'CO' inasimamia Corona, 'VI' kwa virusi na 'D' kwa ugonjwa - ni ugonjwa unaosababishwa na shina mpya ya virusi vya Corona.

Ni nini dalili za COVID-19? Dalili zinaweza kujumuisha:

  • homa
  • kikohozi kavu
  • upungufu wa pumzi
  • uchovu

Katika kesi kali kabisa, maambukizi yanaweza kusababisha nimonia au ugumu wa kupumua. Kwa nadra, ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo.

Dalili hizi ni kama mafua (homa ya mafua) au baridi ya kawaida, ambayo ni kawaida kuliko COVID-19. Hii ndio sababu upimaji unahitajika kudhibitisha ikiwa mtu ana COVID-19. Ni muhimu kukumbuka kwamba hatua muhimu za kuzuia ni sawa - kunawa mikono mara nyingi, kufunika mdomo unapokohoa au kupiga chafya na kiwiko kilichokunjwa au karatasi sashi, kisha kutupa karatasi sashi kwenye pipa iliyofungwa. Pia, kuna chanjo cha mafua- kwa hivyo kumbuka kujiweka mwenyewe na mtoto wako na habari za kisasa kuhusu chanjo.

COVID-19 huenea vipi?

Virusi huenea hasa wakati matone ya mtu aliyeambukizwa (kutoka kwa kukohoa, kupiga chafya, kuongea, kuimba) huingia kwenye mdomo, pua au macho ya walio karibu. Watu wanaweza ambukizwa pia kwa kuguza mdomo, pua au macho yao baada ya kuguza sehemu zilizo na virusi. Virusi vya COVID-19 vyaweza kuishi kwa sehemu kwa masaa chache hadi siku kadhaa ilhali viuaviini rahisi vyaweza kuviua.

Virusi vya COVID-19 vinaweza kupitishwa wakati na kabla ya mtu kuonyesha dalili.

Ifuatayo