Protecting My Family

Ninawezaje ilinda familia yangu kutokana na virusi vya COVID-19?

Zifuatazo ni baadhi ya tahadhari wewe na familia yako mnaeza chukua kujisaidia kuepusha maambukizi:

  • Osha mikono yako mara kwa mara kutumia sabuni na maji ama sanitaiza iliyo na msingi wa pombe
  • Funika mdomo na pua kwa kiwiko kilicho kunjwa ama karatasi ya shashi unapokohoa ama kupiga chafya. Tupa karatasi ya shashi iliyotumika mara moja.
  • Weka angalau umbali wa mita 1 kati yako mwenyewe na wengine.
  • Mara mingi osha na safisha sehemu zinazoguzwa mara kwa mara kama vile simu, komeo la mlango,swichi za mwangaza na sehemu za juu za kaunta.
  • Tafuta matibabu mapema kama wewe ama mtoto wako mna joto jingi, kukohoa, ugumu wa kupumua ama dalili zingine za COVID-19
  • Epuka maeneo yaliyojaa watu, nafasi zilizofungwa na zilizo na uingizaji duni wa hewa na pia jaribu kujizoesha kukaa kwa umbali unaofaa na watu hadharani.
  • Vaa barakoa za kitambaa ukiwa katika maeneo ya umma ambapo kuna maambukizi ya jamii na umbali wa mwili hauwezekani.
  • Weka nafasi zote za ndani zikiwa na hewa nzuri
Iliyotangulia Ifuatayo