Jinsi ya kuzuia kipindupindu
Jikinge na jamii yako
1.Nawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka:
- Baada ya kutumia choo
- Baada ya kumpangusa mtoto kinyesi
- Kabla ya kutayarisha na kula chakula
- Kabla ya kumlisha mtoto.
2.Tumia choo wakati wote unapotaka kujisaidia. Hakikisha choo chako ni kisafi wakati wote. Funga mlango wa choo kila wakati.
- Chimba choo chako umbali wa mita 30 au zaidi kutoka kwa pahali pa kuchota maji.
3.Hakikisha sehemu unayoteka maji ya kunywa imetunzwa vizuri. Kunywa maji ambayo yamechemshwa au kuwekwa dawa.
4.Pika chakula hadi kiive vizuri na ukile kingali moto. Hakikisha vyakula vyote kimefunikwa na kuwekwa vizuri.
- Hakikisha mnakula vyakula vilivyopashwa moto wakati wote
- Hakikisha umeosha matunda na mboga vizuri.