jiko

Unda jiko jua

Jiko jua linalotengenezewa nyumbani ni rahisi sana kuunda!

Lina wastani wa miaka miwili ya kutumika. Wakati huo, linaweza kukuwezesha kuhifadhi tani mbili za kuni, pamoja na kuzuia utoaaji wa mivuke ya dioksidi ya kaboni ambayo ingetolewa ikiwa kuni hizi zingetumika.

Vifaa vya ujenzi:

  • Kadibodi (bodi ya katoni) - mita 0.9x1.2

  • Tepe za aluminiamu- mita 0.3x3, kata vipande vinayohitajika

  • Gundi

  • Burashi ya kupaka rangi (au kifaa kingine cha kutandaza)

  • Kisu cha kawaida au kifaa sawa na hicho cha kukatia

  • Penseli, kalamu au kifaa kingine cha kuchora

Hatua za kuunda:

  1. Chora muundo kwenye kadibod.

  2. Kata umbo.

  3. Onyesha sehemu za kukuja ukitumia kifaa butu, kama mpini wa kijiko. Unda mikunjo iliyonyooka kwa kukunja ukitumia kifaa kigumu kilichonyooka

  4. Kwa kutumia burashi ya kupaka rangi au kifaa kingine cha kutandaza, sambaza mchanganyiko wa gundi/maji kwenye upande wa utepe wa aluminiamu usio na uangaavu, na ubonyeze tepe za aluminiamu zenye gundi kwa nguvu na kwa laini kwa upande ambao utakua sehemu ya ndani ya jiko. Mikunjo kadhaa haina madhara yoyote.

  5. Liache tambarare hadi likauke. Punguza sehemu zozote za ziada.

  6. Sio ya lazima: Funga kingo vizuri ukitumia tepe za gundi. Kwa maelekezo ya kina ya jinsi ya kuunda na kutumia jiko jua, tazama(external link data charges may apply) link

Iliyotangulia