tree

Panda Miti!

1. Ni miti gani ya kupanda?

  • Chagua miti inayofaa kwa hali ya hewa na mchanga wa eneo hilo -ikiwezekana miti ambayo imekuwa ikikua kwenye eneo lako kwa muda mrefu –ili kuwe na uwezekano wa kumea na kukua. Pata mawaidha kutoka kwa mtu wa eneo lako mwenye ujuzi wa miti.

  • Zingatia unachotaka miti ikupe. Kuzuia mmomonyoko wa udongo? Kivuli? Matunda? Kuni? Mandhari ya kuvutia

2. Unafaa kupanda miti lini?

Wakati unaofaa wa kupanda mti kwenye maeneo ya tropiki na maeneo yaliyo ndani ya tropiki ni wakati wa mvua ama wakati usio na mabadiliko ya hali ya hewa. Katika sehemu zenye baridi wakati mwafaka ni mwisho wa majira ya kupukutika baada ya miti kuangusha majani au ya majira ya kuchipua, kabla majani ya miti hayajamea. Hata hivyo, miche iliyo na nguvu na afya inaweza kupandwa wakati wowote wa upanzi.

3. Jinsi ya kupanda?

Miti inaweza kupandwa aidha kama mbegu, sehemu zilizokatwa (kwa aina kadhaa ya miti), miche au miti midogo. Miti midogo ndiyo yenye nguvu na kwa hivyo ina uwezo wa kumea. Kupanda miti midogo:

  • Chimba shimo ambalo upana wake ni mara mbili ya mizizi ya mti ili mizizi iweze kutandaa. Toa mti kutoka kwenye chombo chake. Kata mizizi iliyovunjika kwa makini kisha uufinye mchanga uliozingira mizizi ili uwachane.

  • Weka mti kwenye shimo la kupanda. Kila wakati inua mti kwa kutumia mchanga ulio kwenye mizizi badala ya kutumia shina la mti.

  • Tandaza mizizi ya kando upande wa nje. Usipande mti kimo kirefu chini.

  • Tia kiasi kidogo cha mchanga kwenye shimo la kupanda. Hakikisha kuwa mti uko wima. Jaza mchanga kwa utaratibu. Finyilia mchanga karibu na kitako cha mizizi.

  • Nyunyizia maji vizuri na mchirizi wa maji unaotoka polepole ili mchanga ushikamane.

  • Panga ratiba ya kuuangalia mti huo. Kinga mti huo dhidi ya wadudu na magonjwa kwa kutoa mimea iliyo karibu ambayo inaweza kuudhuru. Kuwa mwangalifu wakati wa misimu ya ukame na unyunyizie maji ikiwa yatahitajika haswa miezi chache ya kwanza.

Iliyotangulia Ifuatayo