garden

Anza bustani shuleni!

Jifunze kuhusu mazingira upate chakula chenye ladha

Shule si tu ya kujifunza wakati wa masomo! Shule ni:

  • Chanzo cha kuboresha chakula na afya ya watoto.

  • Chanzo cha mvuto wa kiafya (kama maji safi ya kunywa, shughuli za kimwili).

  • Eneo la kujifunza (kuhusu asili, kilimo, lishe).

  • Mahala pa burudani na kupumzika.

  • Funzo la kila siku kuhusu kuheshimu mazingira na kujivunia shule yako.

Kuanzisha bustani ya shule kutakusaidia kupata ujuzi unaoweza kutumia, na kupata chakula bora chenye ladha! Unapaswa kuanzia wapi?

  • Jadili mradi wako na mwalimu wako na utafute 'kiongozi wa bustani' (mkuu wa shule au mwalimu mwenye uzoefu) ambaye atakusaidia kuanzisha bustani na kupanga kazi yako.

  • Angalia jinsi viongozi wa elimu, huduma za afya, huduma za kilimo na baraza la mitaa wanaweza kusaidia mradi wa bustani ya shule, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutoa fedha.

  • Husisha watu wanajitolea kukusaidia, kwa mfano kati ya wazazi, wanajamii, wanafunzi na wanafunzi wa zamani wa shule.

  • Tafuta zana na vifaa, mbegu na miche. Gharama isiwe ya juu. Ukianza kwa njia ndogo, kila kitu kinaweza kupatikana kwa miaka michache. Mara nyingi, vifaa vinaweza kukopwa, na unaweza kuhifadhi mbegu zako mwenyewe.

  • Chagua unachotaka kukuza: mimea ya eneo lako, inayofaana na hali ya hewa ya eneo lako, ni nafuu na inaweza kunawiri. Hata kwa bustani ndogo, utakuwa na mafanikio zaidi ikiwa una mazao mbalimbali, sio moja tu au mawili.

  • Mbinu za kiasili ni bora kwa mazingira na hupunguza gharama za mbolea na dawa za kunyunyizia wadudu. Shawishi shule kupitisha maazimio yafaayo.

Katika bustani yetu:

  • Tutaulinda udongo na kuhifadhi maji.

  • Tutatumia mbolea-vunde nyingi na matandazo.

  • Tutapanda mazao kwa zamu.

  • Hatutumii mbolea ya viwandani.

  • Tutaleta takataka ya mahuluku shuleni ili kuunda mbolea-vunde.

-Tutachunguza uwepo wa wadudu kila asubuhi.

Pata maelezo zaidi kuhusu bustani za shule: (external link data charges may apply) Link

Ifuatayo