Mabadiliko ya hali ya hewa huvutia majanga ya asili ya hali ya hewa huvutia majanga ya asili
Ingawa kadiri ya majanga 12 yalitokea kila mwaka katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini, idadi hiyo ilifikia idadi kubwa ya 350 mwaka wa 2004. Kuongezeka kwa ukali wa matukio ya hali ya hewa inayohusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa - kama vile ukame, mafuriko, tufani na vimbunga - kunawahatarisha watu, mara nyingi huharibu maeneo wanayoishi na kufanya kazi na hupelekea uharibifu wa mazao, kuchafuka kwa maji yanayotumika na kugawanyika kwa familia.
Ingawa maafa ya asili yana madhara makubwa kwa mtu yeyote anayekumbana nayo, watoto ndio huathirika zaidi, kwa sababu ya udogo wao na kutoweza kujitunza wenyewe.
Watoto wanaweza kupata maafa zaidi kuliko watu wazima wakati wa majanga ya asili au kupoteza uhai kutokana na utapiamlo, majeraha au magonjwa baadaye.Majanga ya asili yanaweza kulazimisha watoto kuondoka kwenye nyumba zao - au hata nchi zao. Wanaweza kuwa yatima au kutenganishwa na familia zao, na huenda wadhulumiwe na watu wazima walaghai.
Mipango ya kupunguza hatari inapaswa kuundwa ili kuelimisha familia na watoto kuhusu hatua rahisi ambazo zinaweza kulinda maisha na mali binafsi wakati wa majanga ya asili. Programu bora za mafunzo katika shule, nyumbani na katika jamii zinaweza kuleta utamaduni wa kuzuia na uwezeshaji.