Je! Mabadiliko ya hali ya hewa ni nini?

Hali ya hewa ni utaratibu wa hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na misimu, joto la wastani na kali, muda na eneo la mawingu, mvua na theluji, na matukio ya hali ya hewa kali kama vile dhoruba , vimbunga, chamchela na tufani. Hali yetu yaa hewa inabadilika kutokana na mchakato unaojulikana kama 'athari ya gesi zinazoongeza joto'.

Maisha hapa duniani yanawezekana kutokana na nishati kutoka kwa jua, ambayo hutufikia hasa kama mfumo wa mwanga unaoonekana. Dunia huakisi baadhi ya nguvu hizi, na hatimaye huenda angani. Hata hivyo, gesi katika anga hupunguza mchakato huu. Kwa pamoja, gesi hizi zinajulikana kama 'gesi zinazoongeza joto' kwa sababu huzuia joto duniani, kama vile nyumba kitalu ya mkulima hutumika kuhifadhi joto ndani ili kukuza mboga.

Kiasi fulani cha gesi hizi ni muhimu kwetu ili tuishi- bila ya gesi hizi, joto la wastani duniani litakuwa -19° C! Lakini shughuli za kibinadamu (kama shughuli za kilimo na viwanda, na ukataji miti) hufanya blanketi ya gesi zinazoongeza joto kuwa nzito zaidi, na kuongeza athari za gesi zinazoongeza joto.

Kuongezeka kwa joto kutafuatana na mabadiliko katika utandu wa wingu, mvua, mwelekeo wa upepo na muda wa misimu. Tayari tunaona baadhi ya mabadiliko haya.

Kwa sababu mifumo ya hali ya hewa ni tatanishi na inaunganishwa pamoja, mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kumaanisha kwamba baadhi ya sehemu za dunia huwa na upungufu wa joto, wakati sehemu nyingine za dunia zitakuwa na ongezeko la kiwango na, wakati mwingine, idadi ya matukio ya hali ya hewa kali, kama vimbunga, chamchela na dhoruba kali.

Unaweza kutazama video hii ili kuelewa vizuri jinsi inavyofanya kazi: (External link data charges will apply) vimeo.com

Iliyotangulia