9b6d6492778c4ea88a67b7f1246fd2e6

Nitakabilije vitisho?

Mtu fulani ananitumia jumbe za vitisho katika mtandao wa kijamii ambazo zinaniudhi/kasirisha. Nifanye nini?

  • Ikiwa mtu fulani anakutumia jumbe zinazokufanya uudhike au ukasirike yafuatayo ni mambo machache ambayo unaweza kufanya:
  • Mosi, USIMRUDISHIE jumbe za kutisha. Ongea na mtu unayemwamini kuhusu kile kilichotokea na jinsi ulivyojisikia.
  • Endapo unafahamu wahusika unaweza kuzungumza nao ana kwa ana na kuwafahamisha jinsi ujumbe wao ulivyokusabaishia huzuni/maudhi/ hasira.
  • Mitandao mingi ya kijamii inakuruhusu “kuzuia” muhusika asiweze kuwasiliana nawe ili asikutumie tenda jumbe za aina hiyo. Katika mtandao wa Facebook unaweza kubofya kwenye profaili ya muhusika halafu ukabofya kwenye kitufe “zuia” . Mwonekano wa kitufe hiki utategemea aina ya simu unayotumia.
  • Mitandao mingi ya kijamii ina masharti makali dhidi ya utoaji vitisho na maudhi na inakupa nafasi ya kutoa ripoti kuhusu mtu yeyote anayekiuka masharti hayo. Katika mtandao wa Facebook unaweza kutoa taarifa za watu wanaokiuka masharti hayo kwa kuingia katika profaili zao na kubofya “ripoti”.
  • Ikiwa umri wako haujafikia miaka 18 kuna namba maalumu ambazo unaweza kupiga na kuzungumza na mtu fulani kuhusu tatizo lako. Kupiga simu kwa namba hii ni bure. Unaweza kupiga namba hiyo ya watoto ambayo ni 1190.
Iliyotangulia Ifuatayo

Maoni 0