Kuwa mtumiaji namba moja wa intaneti
Vidokezo muhimu zaidi kwa matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii
-
Heshimu mambo yanayosemwa na watu wengine katika mitandao ya kijamii, hata kama hukubaliani nayo.
-
Usichangie na mtu taarifa zako binafsi kama vile anuani, namba ya simu ya kiganjani au taarifa zako za kibenki.
-
Kua mwangalifu unaponunua kitu mtandaoni – nunua tu katika tovuti zinazoaminika.
-
Usipapatikie kitu chochote cha bure mtandaoni – unaweza kuwa ni utapeli. Pakua vitu kutoka katika tovuti zinazoaminika tu.
-
Zingatia kuwa hata vitu vya bure kutoka mtandaoni vinaweza kukugharimu fedha kwa vile hutumia data/ gharama za mtandao.
-
Unaweza kubadili mitegesho ya faragha katika majukwaa yako ya mitandao ya kijamii ili kukusaidia kudhibiti yeyote anayeweza kuona habari na picha zako.
-
Usiamini kila kitu unachosoma mtandaoni kwa mara ya kwanza – tafuta maandiko, tovuti au watu wengine wanaoaminika zaidi na kuona kile wanachosema.
-
Una haki ya kuwa na faragha – na wengine pia. Sio jambo jema kuingia katika akaunti za watu wengine au kutumia simu zao au profaili zao bila ruhusa zao.
-
Usieneze uvumi au kutuma/kuchangia kaitka habari au picha zinazochukiza na kuudhi wengine.Mambo ya utani yanaweza kuwaudhi wengine.
-
Tafakari mara mbili kabla hujabofya ‘tuma’ – hasa kama umehamanika au umekasirika. Utakapokuwa umetuma picha au video kwa watu wengine ni vigumu kudhibiti chochote kitakachofanyika au kitakachoonekana kwa vitu hivyo.
Kinachofuata:
Maoni 2
Tafadhali ingia au fungua akaunti yako
L
Lizz
mwaka 1, miezi 4 ago
L
Lizz
mwaka 1, miezi 4 ago