fbd105b25f2445d8b15e3fcdc28aa199

Uko tayari kiasi gani kutumia Intaneti?

Fanya jaribio!

Jibu maswali yote kwa jibu la Ndio au Hapana – Hakiki jibu lako ulilotoa na tazama mwishoni mwa andiko hili kupata jibu sahihi!

Swali la 1)

Mtu fulani ananitania katika mtandao wa kijamii, ni vyema namimi nimrudishie utani? (Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 2)

Nimeingia katika akaunti ya rafiki yangu kwa dakika mbili tu kutazama jumbe zake, hii ni SAWA? (Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 3)

Mtu fulani ananitumia jumbe za maudhi katika mtandao wa kijamii, ni SAWA kumripoti?

(JIbu Ndio au Hapana)

Swali la 4)

Mtu fulani ninayemfahamu katika Intaneti ananikaribisha kumtembelea kwake, ni SAWA kwangu kumtembelea? (Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 5)

Je jumbe kuhusu kujishindia fedha kwenye intaneti ni utapeli ?

(Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 6)

Nimepokea ujumbe wa mtu nisiyemfahamu wenye anuani ya mtandao, je nibofye na kuingia ili kusoma ujumbe huo? (Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 7)

Je ni RUHUSA kuchangia nywila yangu na mtu ambaye ni rafiki yangu wa karibu sana? (Jibu Ndio au Hapana)

Swali la 8)

Ni sawa kutumia habari za Intaneti katika kazi mradi yangu ya shule ? (Jibu Ndio au Hapana)

Umefaulu kwa kiwango gani? Tazama majibu sasa!

Swali la 1) Jibu ni HAPANA. Usisambaze uvumi au kutuma/kuchangia habari au picha za kuudhi na kukasirisha hata kama mtu fulani amekufanyia hivyo. Kufanya hivyo kutazidi kufanya hali iwe mbaya zaidi. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Tukabilije vitisho?

Swali la 2) Jibu ni HAPANA. Una haki ya kuwa na faragha – vivyo hivyo na watu wengine pia. Sio jambo jema kuingia katika akaunti ya mtu mwingine au kutumia simu au profaili yake bila ruhusa yake. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Ni siri yako

Swali la 3) Jibu ni NDIO. Katika majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii unaweza kutoa ripoti kuhusu habari au picha maalumu endapo inakiuka kanuni za jukwaa la mitandao ya kijamii. Katika Facebook mambo yanayokiuka kanuni ni pamoja na kutoa vitisho, ukatili kwa michoro, utapeli. Tumia kiungo “ripoti” karibu na habari au picha husika kutuma ripoti yako. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Picha/ maudhui ya kuudhi

Swali la 4) Jibu ni HAPANA. Unapaswa kuwa mwangalifu wakati wa kwenda kukutana mara ya kwanza na mtu usiyemjua na ambaye mmefahamiana kupitia intaneti. Siku zote panga mkutane kwenye makutano ya watu wengi (kama kwenye maduka makubwa) na mwambie rafiki au mwanafamilia mahali unakokwenda na mtu unayekusudia kukutana naye. Ni vizuri zaidi kama utamwomba rafiki au mwanafamilia akusindikize. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Kazi hiyo inalipa kweli?

Swali la 5) Jibu ni NDIO. Kama unatumia intaneti upo uwezekano mkubwa wa kupokea barua pepe au ujumbe kukujulisha kuwa umejishindia fedha, au tuzo kama vile simu au safari ya mapumziko. Ujumbe wa aina hiyo ni utapeli na usiuamini kabisa. Uwezekano ni mdogo sana kwamba utakuwa umejishindia kitu fulani kama hukuwahi kushiriki mashindano yoyote. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Kupokea ujumbe wa kujishindia fedha

Swali la 6) Jibu ni HAPANA. Usibofye katika viungo ndani ya barua pepe iliyotoka kwa mtu usiyemfahamu. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Kupokea ujumbe wa kujishindia fedha?

Swali la 7) Jibu ni HAPANA. USIDHUBUTU kuchangia nywila yako na mtu mwingine. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Ni siri yako

Swali la 8) Jibu ni HAPANA. Intaneti ina habari nyingi zinazofaa kwa kazi za masomo na kazi mradi. Kwa kawaida unaanza kwa kuandika jina pamoja na maelezo ya chanzo cha habari katika marejeo ya kazi mradi ya shule/ chuo kikuu. Hata hivyo hairuhusiwi kutumia kazi ya mtu mwingine iliyoko kwenye intaneti na kudanganya kuwa ni yako mwenyewe. Ungependa kufahamu zaidi? Soma: Kutumia intaneti katika masomo/kazi mradi

Umepata kuanzia swali 1- 4 ? Ni vizuri lakini sio vizuri sana. Bado una nafasi ya kufanya vizuri zaidi, soma tena habari zote katika Smart Connect, fanya tena jaribio na uone jinsi utakavyokuwa umefanya vizuri zaidi sasa.

Umepata kati ya maswali 5 - 7 ? Vizuri sana, kidogo ungepata yote! Soma kwa makini mada ya swali ulilokosa kisha rudia tena jaribio!

Umepata Maswali yote 8 ? Unatisha, wewe ni kiboko cha Intaneti! Wafahamishe marafiki zako na wape jaribio hilo wafanye. Wako tayari kiasi gani kutumia intaneti?

Kidokezo cha intaneti kinachofuata:

Maoni 0