how often

Nitapata hedhi mara ngapi?

Mzunguko wa hedhi ni hatua nyingi asilia ambazo wasichana na wanawake hupitia ili kuwatayarisha kupata mimba. Kemikali za kawaida zinazotengenezwa mwilini mwako ambazo zinaitwa homoni, hudhibiti kipindi cha hedhi yako na huongezeka na kupunguka kulingana na mahali ulipo katika mzunguko wa hedhi.

Menstrual Cycle

Mizunguko mingi ya hedhi hudumu takribani siku 28, lakini wakati mwingine huwa mifupi (hadi siku 21) au mirefu (hadi siku 35). Ni muhimu uelewe kuwa (jinsi vilivyo vitu vingi) miili ya watu huwa tofauti, kwa hivyo urefu wa mizunguko pia huwa tofauti.

Tuzungumzie kipindi cha hedhi yako:

  • Siku ya kwanza ya kuvuja damu ndiyo mwanzo wa mzunguko wa hedhi. Hii hutokea wakati utando wa ndani wa uterasi inapasuka na kuanza kuvuja damu.

  • Wiki mbili baadaye ostrojeni na testosteroni huongezeka na mayai hukomaa. Utaratibu huu wa siku 13 husababisha kukua upya kwa endometrimu (utando wa ndani wa uterasi) ili kukutayarisha kupata hedhi inayofuata.

  • Katika siku ya 14, yai ambalo limekomaa hutolewa kwenye ovari yako moja na ikiwa halijarutubishwa, litaondolewa baada ya siku moja.

  • Siku chache baadaye, huenda upate hisia zinazokufanya unune kidogo na huenda pia ukapata dalili ndogo za hisia za kabla ya hedhi (PMS).

  • Katika wiki ya nne, utafikia awamu ya lutiemu. Awamu hii hufanya utando wa ndani wa uterasi kuwa mkubwa na iwapo hamna yai lililorutubishwa, utapasuka na kuvuja damu ya hedhi.

Jinsi ulivyo mzunguko wa hedhi, Dalili za Kabla ya Hedhi (PMS) na ishara zake hutofautiana kulingana na watu. Kabla ya hedhi au wakati wa hedhi, huenda ukapata maumivu ya kichwa, kitefutefu, kufura kwa tumbo, kuumwa na matiti, na mabadiliko mengine ya mwili. Wewe ndiwe unayefaa kufafanua na kutabiri hisia hizi. Pia kumbuka kujitunza vizuri kila mara.

Njia bora ya kufuatilia mzunguko wako wa hedhi ni kuhesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi wakati itakaporejea tena

Ifuatayo