Bleeding

Kwa nini ninavuja damu?

Kupata hedhi ni jambo la kawaida. Hali hii hutokea takribani kila mwezi kwa wasichana na wanawake bilioni 1.8 duniani kote. Kwa wasichana wengi, hedhi huanza kati ya umri wa miaka 10 na 15.

Reproductive System

Katika kipindi cha hedhi, kiasi kidogo cha damu huvuja kwenye uuke wako kwa takribani siku tatu hadi saba. Damu hiyo hutoka kwenye tumbo la uzazi (uterasi). Wasichana wote hupata hedhi wakiwa katika harakati ya kuwa watu wazima. Wakati unavuja damu, inamaanisha kuwa kiungo chako cha uzazi kinafanya kazi na unaweza kupata mimba (ukifanya ngono). Ili kudumisha afya ya wanawake na watoto, ni muhimu mwanamke asubiri hadi awe mtu mzima kabla ya kupata mtoto. Ingawa hedhi inaweza kutisha mara ya kwanza na ni lazima uipate kila mwezi, ni vyema kukumbuka kuwa kupata hedhi kunamaanisha kuwa una afya na mwili wako unakua vizuri.

Iliyotangulia