101 Image

Hedhi 101

Je, hedhi ni nini?

Hedhi ni kazi ya asili ya mwili ambayo inawaruhusu wanawake kupata mimba na kupata watoto. Wakati wa hedhi yako, damu kutoka kwa uterasi (tumbo la uzazi) hupitia kwenye uke na kutoka nje ya mwili. Hedhi ni jambo la kawaida kabisa na la kiafya!

Kwa nini wasichana hupata hedhi?

Hedhi ni sehemu ya mfumo wa uzazi. Mfumo wa uzazi unaundwa na sehemu za mwili zinazowezesha watu kupata watoto.

Katika kila mzunguko wa hedhi, utando wa uterasi yako hujiandaa kwa yai lililorutubishwa kwa kuwa mnene ukiwa umejazwa damu na tishu. Ikiwa yai litarutubishwa na manii, yai lililorutubishwa hupandikizwa kwenye utando huu na kukua na kuwa mtoto. Lakini ikiwa hakuna yai lililorutubishwa, basi utando huo huambuliwa kupitia uke wako.

Nitapata lini hedhi yangu ya kwanza?

Kwa kawaida hedhi za wasichana huanza wakiwa kati ya umri wa miaka 9-15, takriban miaka miwili baada ya matiti yao kuanza kukua.

Kwa kawaida wanawake huacha kupata hedhi kati ya umri wa miaka 45 na 55.

Nitapoteza damu kiasi gani?

Huenda ikaonekana kuwa nyingi, lakini huwa takribani vijiko vitatu vya kulia chakula kwa jumla. Wasichana na wanawake wengi huanza na mtiririko mzito mwanzoni mwa hedhi yao na kumalizia mtiririko mwepesi.

Itakuwaje iwapo sina kifaa cha hedhi na niko mbali na nyumbani?

Iwapo mwalimu au rafiki wa kike hawezi kukusaidia, unaweza kukunja karatasi ya shashi pamoja ili utengeneze sodo ya muda na uiweke kwenye chupi yako. Hii haitadumu kwa muda, lakini inaweza kukusaidia kabla ya kupata kifaa kilicho bora.

Je, watu watajua kuwa ninapata hedhi?

Hapana. Isipokuwa uamue kusema, hakuna atakayejua kuwa unapata hedhi kwa sababu hakuna dalili za hedhi zinazoonekana na mtu yeyote. Hata hivyo, ni vizuri umwambie mwanafamilia au rafiki ikiwa ni mara yako ya kwanza kupata hedhi na unahitaji usaidizi.

Hedhi yangu itadumu kwa muda gani?

Kwa kawaida, hedhi hudumu kati ya siku mbili na saba lakini zinaweza kuchukua muda mrefu zaidi.

Ninaweza kuenda shuleni na kushiriki michezo?

Ndiyo! Hakuna sababu ya kukosa kuenda shuleni au kuacha kushiriki michezo kama kawaida. Hakikisha tu kuwa umebeba vifaa vya hedhi iwapo utahitaji kuvibadilisha ukiwa shuleni.

Bado sijaanza kupata hedhi! Ninapaswa kufanya nini?

Hakuna anayefanana na mwingine na miili yetu hukua katika kasi inayotofautiana. Hili si tatizo na unaweza kuzungumza na mwalimu wa kike akusaidie uelewe kinachotendeka. Tunakushauri umwone daktari tu ikiwa umefikisha umri wa miaka16 na hujaanza kupata hedhi; iwapo kipindi chako cha hedhi kitadumu kwa zaidi ya siku saba au zaidi; au ikiwa hedhi yako itaanza na kukoma ghafla.

Kuna tofauti gani kati ya sodo zinazoweza kutupwa na pedi za nguo?

Sodo zinazoweza kutupwa hutumika mara moja kisha kutupwa, ilhali pedi za nguo zinaweza kutumiwa, kusafishwa na kutumika tena wakati zimekauka.

Je, ninahitaji kumwona daktari wakati ninaanza kupata hedhi?

Hapana. Kupata hedhi ni jambo la kawaida.

Sipati hedhi mara moja kwa mwezi kama wasichana wengine. Ninastahili kufanya nini?

Idadi ya siku kati ya hedhi zako inaweza kutofautiana, hasa katika miaka michache ya kwanza ya hedhi. Hili ni jambo la kawaida na la kiafya. Ikiwa una intaneti na simu mahiri, unaweza kufuatilia na kujifunza jinsi ya kutabiri mzunguko wako wa hedhi kupitia programu ya OKY

Iliyotangulia Ifuatayo