What should I do?

Hedhi yangu imeanza! Ninapaswa kufanya nini?

Ninapata hedhi mara ya kwanza na sijui kitakachofanyika. Ninapaswa kufanya nini kwanza?

W2 bottom

Hedhi yako ya kwanza ni ishara ya mabadiliko ya kawaida ya kimwili na hupaswi kuwa na hofu yoyote. Kwa kuwa ni mara yako ya kwanza, mwambie mzazi, ndugu mkubwa, rafiki au mwalimu unayemwamini. Wataweza kukupa maelezo na vifaa vya hedhi unavyohitaji.

Girl top dialogue 2

Je, ninabakije msafi wakati wa hedhi?

W2 bottom

Hedhi inaweza kuwa na uchafu mwingi, hasa ikiwa itaanza wakati hukuwa unaitarajia! Lakini kumbuka kwamba huu ni mchakato wa kiasili. Kudumisha usafi ni rahisi:

  • Osha nje ya uke wako (na mapaja kama yana damu) kwa maji safi mara moja au mbili kwa siku, kama unaweza.
  • • Fua nguo yoyote iliyochafuliwa kwa maji baridi na sabuni.
  • Badilisha pedi, kitambaa au kisodo mara tu kinapojaa ili kuzuia uvujaji (kwa visodo, badilisha angalau kila saa 4-8).
  • Kamwe usijaribu kuosha sehemu ya ndani ya uke wako kwa maji, sabuni au bidhaa nyingine yoyote.
Girl top dialogue 2

Inaonekana kuwa si rahisi kutumia vifaa vya hedhi. Nitajuaje kifaa kinachonifaa?

W2 bottom

Usitisike. Vifaa vya hedhi vinaboreshwa kila wakati na vipo ili kurahisisha maisha yako. Kutegemea upatikanaji katika duka la dawa au duka kuu, kuna aina nyingi za vifaa vya hedhi kama vile sodo, tamponi, kikombe cha hedhi, au pedi za nguo zinazotumiwa mara moja na zinazoweza kutumiwa tena. Unaweza kujaribu aina zote kisha uamue aina ambayo inakufaa. Pia, unaweza kuchanganya aina mbalimbali, kulingana na uzito wa damu ya hedhi katika siku fulani.

Girl top dialogue 2

Kumbuka...

  • Kama kawaida, nawa mikono yako kabla ya kuondoka msalani na baada ya kubadilisha kifaa cha hedhi.
  • Usitupe kifaa cha hedhi kwenye choo cha maji kwa sababu unaweza kuharibu mfumo wa maji taka. Kabla ya kukitupa kwenye pipa taka, kifunge kwa karatasi ya shashi.
  • Baada ya kipindi fulani, mzunguko wako wa hedhi utakuwa na utaratibu fulani na utaweza kuufuatilia kwa urahisi. Kwa sasa, hakikisha kuwa una vifaa vya hedhi katika mkoba wako kwa kuwa inaweza kuanza wakati wowote.
Iliyotangulia Ifuatayo