Kwa nini ninavuja damu?
Kupata hedhi ni jambo la kawaida. Hali hii hutokea takribani kila mwezi kwa wasichana na wanawake bilioni 1.8 duniani kote. Wasichana wengi hupata hedhi kwa mara ya kwanza kati ya umri wa miaka 10 na 15.
Katika kipindi cha hedhi, kiasi kidogo cha damu huvuja kwenye uke wako kwa takribani siku tatu hadi saba. Damu hiyo hutoka kwenye tumbo la uzazi (uterasi). Unapopata hedhi ya kwanza, ina maana kwamba kiungo chako cha uzazi sasa kinafanya kazi na unaweza kuwa mjamzito (ukishiriki ngono). Ili kudumisha afya ya wanawake na watoto, ni muhimu mwanamke asubiri hadi awe mtu mzima kabla ya kupata mtoto.
Ingawa hedhi inaweza kutisha mara ya kwanza na ni kitu ambacho lazima ukidhibiti kila mwezi, ni vyema kukumbuka kuwa kupata hedhi kunamaanisha kuwa una afya na mwili wako unakua vizuri.