a3f115bfdeb34a349cf2b3cf6d61f554

Kuongea na watoto kuhusu usalama wa intaneti?

Watoto wangu hutumia intaneti na mitandao ya kijamii na nina wasiwasi – nifanye nini?

  • Jambo zuri zaidi la kufanya ni kuongea na watoto wako ili uweze kufahamu aina ya matumizi yao ya intaneti na mitandao ya kijamii.
  • Waulize kuhusu aina ya tovuti wanazotumia na aina ya habari wanazotafuta. Waombe wakufahamishe ni habari zipi wanazipenda na zipi hawazipendi katika intaneti.
  • Zungumza nao kuhusu tabia wanazoziona kuwa ni nzuri na zile wanazoziona kuwa ni mbaya katika intaneti na mitandao ya kijamii.
  • Ni muhimu kuwa na mazungumzo ya ana kwa wana na watoto wako ili wawe huru kukueleza kuhusu mambo wanayofanya mtandaoni na pia waweze kukueleza kama wameshakutana na jambo la kuwaudhi katika intaneti.
  • Waombe watoto wako wakusaidie uweze kujifunza zaidi masuala ya utumiaji wa intaneti. Watoto wengi wanajua vizuri sana jinsi ya kutumia intaneti na wanaweza kukusaidia katika kujifunza zaidi.

Kidokezo cha intaneti kinachofuata:

Iliyotangulia Ifuatayo

Maoni 0