Kutumia intaneti katika kazi mradi
Ninafanya utafiti kwa ajili ya shule/chuo kikuu – nawezaje kutumia intaneti katika kazi hii?
- Intaneti ina habari nyingi zinazoweza kusaidia katika kazi za masomo na za utafiti. Unaweza kutafuta habari hizo kwa kutumia injini pekuzi au Wikipedia, anza kwa kuandika neno kuu la kudokeza mada unayotafuta.
- Endapo unatafuta habari kwa ajili ya kazi ya shule au chuo kikuu itakubidi wakati wote utafute mwandishi wa habari unayotafuta (hufahamika pia kama “chanzo” au “rejeo”).
- Chanzo/Rejeo zuri kwa ajili ya kazi mradi ya shule /chuo kikuu ni pamoja na: vyuo vikuu, majarida ya kitaaluma, tovuti za mashirika makubwa, ripoti rasmi nk.
- Orodhesha tovuti zote ulizotumia kukusanya habari
- Bila shaka itakubidi uingize orodha hiyo katika orodha ya marejeo ya kazi mradi yako.
- Kwa kawaida unaanza kwa kuandika jina pamoja na maelezo ya chanzo cha taarifa katika marejeo ya kazi mradi ya shule/ chuo kikuu.
- Chunguza wakati habari uliyopata ilipoandikwa ili ujue kama ni ya zamani - unaweza kupata habari mpya. Zingatia kwamba habari kama za kitakwimu hubadilika mara kwa mara.
- Zingatia kwamba sio kila habari utakayopata kwenye intaneti ni ya kweli – kuwa mwangalifu na aina ya vyanzo vya habari unavyoviamini.
Kidokezo cha intaneti kinachofuata:
Maoni 0
Tafadhali ingia au fungua akaunti yako
Nakala zinazohusiana
Kuongea na watoto kuhusu usalama wa intaneti?
Ni siri yako
Kuwa mtumiaji namba moja wa intaneti
© The Internet of Good Things