Unamfahamu mtu anayekuingiza?
Mtu fulani alinitumia ombi la urafiki – lakini simfahamu mtu huyo, napaswa nifanye nini?
- Wakati mwingine watu hupenda kuwa na mawasiliano ya kimtandoa na marafiki wengi katika mitandao ya kijamii hivyo watu hao hutuma maombi mengi ya urafiki kwa watu wasiowafahamu.
- Kabla hujakubali ombi la mtu unapaswa kwanza kupitia profaili (sifa) zao – jaribu kubaini watu hao ni akina nani. Kuna marafiki zako wanaowafahamu? Mnatoka katika mji mmoja?
- Usiwakubalie maombi yao kama hupo tayari kushirikiana nao taarifa zako binafsi.Usijione kama unalazimishwa kufanya hivyo.
- Hakikisha unakoweka taarifa zako binafsi ni salama ili mtu wa aina hiyo asiweze kuzipata endapo hupendi azipate.
- Zingatia pia kuwa wakati mwingine katika intaneti watu hudanganya ili waonekane tofauti na walivyo.
Kidokezo cha Intaneti kinachofuata:
Maoni 0
Tafadhali ingia au fungua akaunti yako
Nakala zinazohusiana
Nitakabilije vitisho?
Picha/maudhui ya kuudhi
Kazi ninayoitiwa ipo kweli?
© The Internet of Good Things