Kazi ninayoitiwa ipo kweli?
Mtu fulani amenitumia ujumbe wa kuniitia kazi. Wamenitaka nikutane nao ana kwa ana. Nifanye nini?
- Uliwahi kuomba kazi au kuzungumza na mtu yeyote kuhusu kazi? Kama hukuwahi kufanya hivyo, huo unaweza kuwa ni ujumbe wa kitapeli – kuwa mwangalifu.
- Chunguza kidogo kuhusu kampuni au shughuli unayoitiwa – tafuta taarifa hizo kwenye intaneti au muulize rafiki yako.
- Unapaswa kuwa mwangalifu pale unapokwenda kukutana kwa mara ya kwanza na mtu usiyemjua na ambaye umemfahamu kupitia Intaneti.
- Siku zote panga mkutane sehemu yenye makutano ya watu (kama kwenye maduka makubwa).
- Siku zote mfahamishe rafiki yako au mwanafamilia kuhusu mahali unakokwenda na mtu unayekwenda kukutana naye.
- Ni vyema zaidi kama utamwomba rafiki yako au mwanafamilia akusindikize.
Kidokezo kinachofuata kuhusu Intaneti:
Maoni 0
Tafadhali ingia au fungua akaunti yako
Nakala zinazohusiana
Picha/maudhui ya kuudhi
Unamfahamu mtu anayekuingiza?
Kuwa mtumiaji namba moja wa intaneti
© The Internet of Good Things